Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mojawapo ya mafunzo muhimu zaidi katika Uislamu ni uaminifu na kulinda amana. Qur’ani Tukufu inasema:
«إِنَّ اللَّهَ یَأْمُرُکُمْ أَنْ تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَیٰ أَهْلِهَا.»“Hakika Mwenyezi Mungu anawaamrisha mzirejeshe amana kwa wenyewe.” (1)
Sherehe:
Mada ya uaminifu inaweza kuangaliwa katika nyanja mbili kuu:
1. Amana za kidunia, zile ambazo watu wanapeana wao kwa wao.
2. Amana za kiroho, ambazo Mwenyezi Mungu amemkabidhi mwanadamu, kama vile akili, dini, au wajibu wake.
Aina zote mbili zina nafasi kubwa sana katika Uislamu.
Amana za Kidunia:
Umuhimu na uzito wa amana za kidunia uko katika kutekeleza au kulinda amana, hakuna tofauti kama ikiwa mwenye amana hiyo ni rafiki au adui.
Imam Sajjad (as) anasema:
«عَلَیکمْ بِاداءِ الاْمانَةِ فَوالَّذِی بَعَثَ مُحَمّداً(صلی الله علیه وآله) بِالحَقِّ نَبِیاً لَوْ اَنَّ قاتِلَ اَبِی الْحُسَینِ ابْنِ عَلِی(علیه السلام) اَئْتَمَنَنِی عَلَی السَّیفِ الَّذِی قَتَلَهُ بِهِ لاَدَّیتُهُ اِلَیه.»
“Wajib kwenu kurudisha amana kwa wenyewe. Naapa kwa Yule aliyemleta Muhammad (saww) kwa haki kuwa Nabii, lau muuaji wa baba yangu Hussein (as) angenikabidhi upanga alioutumia kumuua baba yangu kama amana, ningerudisha amana hiyo kwake bila khiyana.” (2)
Katika mwaka wa saba Hijria, wakati wa vita vya Khaybar, chakula cha jeshi la Kiislamu kiliisha. Wakiwa na njaa kali, walikuwa wakila nyama kama Farasi na nyengine ambazo ni makuruhu, katika hali ile walimuona mchungaji aliyekuwa anachunga kondoo wa Mayahudi. Walitaka kuwachukua kondoo hao kama ngawira, lakini mchungaji alisema: “Hawa ni amana mikononi mwangu.”
Mtume (saww) akasema kwa uwazi mbele ya mamia ya askari wenye njaa:
“Katika dini yetu, kukhini amana ni miongoni mwa dhambi kubwa zaidi. Wajibu wako ni kuwarudisha kondoo hawa kwa wamiliki wao.”
Mchungaji huyo akaamua kusilimu, akawarudisha kondoo kwa wamiliki wao, kisha akaungana na jeshi la Kiislamu, akapigana hadi akauawa shahidi. (3)
Kipimo cha Kuwatambua Watu:
Miongoni mwa vigezo ambavyo Imam Sadiq (as) amevieleza ili kumtambua mtu wa kweli, ni uaminifu. Amesema:
«لاَ تَنْظُرُوا إِلَی طُولِ رُکُوعِ اَلرَّجُلِ وَ سُجُودِهِ، وَ لَکِنِ اُنْظُرُوا إِلَی صِدْقِ حَدِیثِهِ وَ أَدَاءِ أَمَانَتِهِ.»“Msitazame mtu kwa muda mrefu wa rukuu na sajda zake, bali tazameni ukweli wa maneno yake na uaminifu wake katika kurudisha amana.” (4)
Kazi na Majukumu ya kila mtu ni Amana
Uaminifu hauishii kwenye mali pekee. Kila jukumu au nafasi ambayo mtu amepewa ni amana mikononi mwake. Anatakiwa ailinde na kuitekeleza kwa uadilifu.
Imam Ali (as) aliandika barua kwa Ash‘ath ibn Qays, gavana wa Azerbaijan, baada ya vita vya Jamal:
«إِنَّ عَمَلَکَ لَیْسَ لَکَ بِطُعْمَةٍ وَ لَکِنَّهُ فِی عُنُقِکَ أَمَانَةٌ.»
“Cheo chako si riziki ya kujinufaisha, bali ni amana shingoni mwako.” (5)
Kama viongozi na wenye dhamana zote katika jamii wangechukulia majukumu yao kwa mtazamo huu, matatizo mengi yangetatuliwa bila hata shinikizo.
Imam Ali (as) anasema:
«مَنْ لاَ أَمَانَةَ لَهُ لاَ إِیمَانَ لَهُ.»
“Yule asiye na uaminifu, hana imani.” (5)
Rejea:
1- Surat an-Nisa, aya ya 58
2- «عَلَیکمْ بِاداءِ الاْمانَةِ فَوالَّذِی بَعَثَ مُحَمّداً(صلی الله علیه وآله) بِالحَقِّ نَبِیاً لَوْ اَنَّ قاتِلَ اَبِی الْحُسَینِ ابْنِ عَلِی(علیه السلام) اَئْتَمَنَنِی عَلَی السَّیفِ الَّذِی قَتَلَهُ بِهِ لاَدَّیتُهُ اِلَیه.» مشکاةالانوار طبرسی، ج ۳، ص ۱۴۲.
3- Rejea: Sira Ibn Hisham, juzuu ya 3, uk. 345; Furugh Abadiyyat, juzuu ya 2, uk. 247.
4- «لاَ تَنْظُرُوا إِلَی طُولِ رُکُوعِ اَلرَّجُلِ وَ سُجُودِهِ، وَ لَکِنِ اُنْظُرُوا إِلَی صِدْقِ حَدِیثِهِ وَ أَدَاءِ أَمَانَتِهِ.» کافی، ج ۲، ص ۱۰۵.
5- Nahjul-Balagha, barua namba 5
6- Ghurar al-Hikam, juzuu ya 1, uk. 587
Imetayarishwa katika idara ya Elimu na Utamaduni ya Shirika la Habari la Hawza.
Maoni yako